NI MOJA YA Staa wa Bongo Movies na Bongo Fleva, Baby Madaha amesema ukimya wake umesababishwa na uamuzi wake wa kuingia kwenye filamu na kuwa mzalishaji.
Baby amesema ameamua asiwe mtu wa kutegemea kuimba na kufanya filamu tu, bali pia ajishughulishe na shughuli nyingine.
“Kiukweli muziki wa sasa hivi una changamoto kubwa sana, wasanii wachanga wameibuka na wanafanya vizuri sana. Kama mimi ninazo kazi nyingi ila sasa hivi nimeamua nisifanye muziki na filamu pekee. Nimefungua kampuni yangu ambayo inafanya production ya filamu na vitu ngingine. Pia mimi licha ya kuwa muimbaji na muigizaji nataka kuwa producer wa filamu. Yaani ni mtu ambaye nafanya mambo mbalimbali zaidi ya muziki na filamu,” Baby Madaha ameiambia Bongo5.
Katika hatua nyingine muimbaji huyo amezungumzia mahusiano yake na label ya Candy & Candy ambayo iliyokuwa ikimsimamia.
>>Sasa hivi Tanzania kwa sababu nina kampuni yangu mwenyewe na inahitaji usimamizi, mimi na Candy & Candy bado tuna mkataba na unaisha mwezi wa tisa. Lakini uwepo wangu mimi huku wameuridhia na kama wananihitaji kikazi nitaenda. Kwahiyo sioni haja ya kukaa Kenya wakati sifanya kitu chochote wakati naweza kukaa hapa nikazalisha kazi kupitia kampuni yangu mwenyewe chini ya baraka zote za Candy & Candy. Kwahiyo kila kitu kinaenda sawa.<<
0 comments:
Post a Comment