+10 344 123 64 77

Friday, June 5, 2015

KWENYE MICHEZO!!! MSHAMBLIAJI WA KIMATAIFA FALCAO KUHAMIA CHELSEA............FUATILIA

0678439001429626292_filepicker


NI Mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia Radamel Falcao Garcia anatarajiwa kuendelea kubaki nchini England kwenye ligi kuu ya soka nchini humo akiwa na klabu ya Chelsea ambayo siku chache zijazo inatarajia kuthibitisha kumsajili kwa mkataba wa mkopo wa msimu mzima .
Falca0 ambaye msimu uliopita aliiwakilisha Manchester United ambako hata hivyo hakuweza kuonyesha cheche zake atajiunga na timu hiyo ya Lond0n kwa mkataba wenye thamani ya Euro Milioni 7 huku Chelsea ikiwa na chaguo la kumsajili moja kwa moja endapo itaridhika na kiwango chake .
Wakala wa Falcao Jorge Mendes amekuwa jijini London kukamilisha masuala kadhaa yaliyozunguka usajili wa mshambuliaji huyo na ndani ya siku chache zijazo anatarajia kuthibitishwa rasmi kama mchezaji wa Chelsea .
Falca0 atakuja kuziba pengo la Didier Dr0gba ambaye ameihama klabu hiyo baada ya kurudi kwa mara ya pili ambapo amecheza kwa msimu mmoja na kuisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya England .

0 comments:

Post a Comment