NI Staa wa bongo movies, Steve Mengere ‘ Steve Nyerere’ amesema hana mpango na shutuma mbalimbali zinazosemwa na baadhi ya wasanii wenzake kwani Mungu atamlipa kutokana na uvumilivu wake
Steve nyerere aliyasema hayo na kuweka wazi kuwa kuna watu wanamchafua ambao hawana ishu yoyote hapa mjini zaidi ya kutupia picha kwenye mitao ya kijamii na kujinadi kwa nyumba nzuri na na magari ya kuazima.
>>>>Unajua kuna mambo kibao ya kufanya katika jamii lakini watu hawayaoni zaidi ya majungu tu hao watu hawana la kufanya katika maisha yao wao ni kuwaza tu sherehe itafanyika lini ili wafike mapema na kuwafunika hata wanakamati <<< alisema Steve Nyerere.
Alizidi kuhoji Steve Nyerere kuwa kila kukicha anazidi kuchafuliwa bila kuelewa ni nini kinaendelea na kama kuna tatizo kubwa aulizwe kuliko kusimangwa bila mpango.
Mungu atanilipia kwa kweli kwa yote wanaonnipangia hayatanifika ila nataka kusema hivi majunguhayana maana yoyote kusingiziana mamba ambayo hayana maana na kuchafuliana majina bila ya mpangilio” aliongeza Steve.
0 comments:
Post a Comment