NI Usiku wa kuamkia jana jumatatu kituo cha polisi cha Stakishari kilichopo, Ukonga,Dar es salaam kilivamiwa na majambazi na kusababisha vifo vya askari wanne, raia wawili na jambazi mmoja.
Hekaheka ilifunga safari na kwenda katika kituo hicho na kukutana na watoto watatu ambao walikuwa wamepotea na kupelekwa kituoni hapo ili wakutanishwe na ndugu zao na wadai walishuhudia majambazi hao wakiua watu.
Mbali ya watoto hao kupotea taharuki iliyosambaa eneo hilo ni kuhusiana na jambazi aliyeuawa kufananishwa na mwendesha bobadoda wa eneo hilo na kuzua maswali kwa wakazi wa hapo.
0 comments:
Post a Comment