+10 344 123 64 77

Wednesday, August 5, 2015

JOHARI........SASA NIMEMPATA MRITH WA REY KATIKA FILAM ZA BONGO...BOFYA KUJUA ZAIDI HAPA

Blandina William Wilbert Chagula ‘Johari’.

Blandina William Wilbert Chagula ‘Johari’, hatimaye ameondokana na maumivu ya kimapenzi kutoka kwa aliyekuwa mwandani wake, Vincent Kigosi ‘Ray’ baada ya kumpata mwanaume anayeamini ndiye mumewe mtarajiwa.

Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni ndani ya Jengo la Dar Free Market jijini Dar, mmoja wa watu wa karibu na Johari, ambaye pia ni msanii wa kike mwenye jina kubwa (licha ya hivi karibuni kutoigiza mara kwa mara) na kwa sharti la kuhifadhiwa jina lake, alisema Johari amepata mwanaume ambaye ni mtumishi wa serikali na muda wowote wanatarajia kutangaza ndoa.

Ray.
‘Kikulacho’ huyo wa Johari alisema, kwa muda mrefu Johari amekuwa akipitia mateso makali ya moyo baada ya kutendwa vibaya na Ray kwa kuanzisha uhusiano na Chuchu Hans licha ya kwamba wametoka mbali kimapenzi.
Rafiki huyo wa Johari alizidi kumwaga ubuyu kuwa katika kusaka faraja, staa huyo alijikuta amenasa katika mahaba ya mwanaume huyo na kuweka sawa mipango yote ikiwemo kutambulishana nyumbani na muda wowote watafunga ndoa.

“Ila naomba kabisa usinitaje, maana Johari hapendagi mambo yake binafsi yawe wazi, ana mwanaume wanayependana sana, ni mfanyakazi wa serikali.
“Wameshatambulishana hadi kwa wazazi, walikutana kipindi cha Johari akiwa na mawazo ya kuachwa na Ray, tena walikutana kwenye baa ya (akaitaja jina) pale Sinza, na kwa sasa Johari anafurahia mapenzi, jamaa mwenyewe anajulikana kwa jina la Martin,” alisema shosti huyo wa Johari.
Baada ya kumwagiwa ‘ubuyu’ huo, mwandishi wetu alichukua jukumu la ‘kusaga lami’ hadi ofisini kwa Johari, Sinza- Mori jijini Dar na kumtaka aweke bayana kuhusu penzi lake jipya ambapo alijibu kwa staili ya ‘kuingia na kutoka’.

“Aah, nani amekwambia habari hizo? Sipendi sana kuzungumzia mambo yangu binafsi sasa hata kama ni kweli kwani tatizo liko wapi? Mimi si mwanamke? Nilitarajia utaniuliza juu ya ujio wa filamu yangu ya True Love Never Die, wewe unakomalia mambo binafsi tu,” alisema Johari huku akiomba aachwe kwani alikuwa bize  na kazi

0 comments:

Post a Comment