Johnny Strange kutoka Uingereza, umri wake ni miaka 26, jina lake linaandikwa kwa wino mzito kwenye Kitabu cha Kumbukumbu kubwa Duniani, Guinness World Records baada ya kuandika Rekodi ambayo watu wengi wamebaki vinywa wazi wakimshangaa.
Strange kayafanya maajabu yake na Dunia itamkumbuka kwa rekodi nyingi alizowahi kuziandika ikiwemo hii mpya ya kuvuta ndege kwa kutumia masikio yake !!… YES, haikuwa kazi rahisi kwake lakini tayari ameikamilisha na Rekodi yake imeingizwa kwenye Kitabu cha Kumbukumbu za Guinness cha mwaka 2016.
‘Haikuwa kazi rahisi kufanikiwa kuandika Rekodi hii… Ninafurahia sana kuandika Rekodi mpya kila wakati na jina langu kuandikwa kwenye Kitabu cha Guinness, yani mpaka nakosa sehemu ya kutundika vyeti vyangu sasahivi‘– Johnny Strange.
Ndege ambayo jamaa kaivuta ina uzito wa Kilo 670, na amefanikiwa kuivuta Ndege hiyo kwa umbali wa kama Mita 20 hivi… hii inakuwa ni mara ya nane kwake kuvunja rekodi na jina lake kuingia kwenye Kumbukumbu za Kitabu cha Guinness, rekodi ya kwanza aliivunja akiwa na umri wa miaka 10 tu.
Kipande cha Video chenye story yake hiki hapa mtu wa nguvu, Strange na maajabu yake yani !!
0 comments:
Post a Comment