+10 344 123 64 77

Thursday, October 1, 2015

LULU......NI BONGE LA SIRI MIMI NA DOKTA!!!!

MUDA  Chache baada ya muigizaji wa siku nyingi, Mahsein Awadhi Said ‘Dk. Cheni’ kutoa tamko juu ya kumuoa ‘mtoto mkubwa’ katika tasnia hiyo, Elizaberth Michael Kimemeta ‘Lulu’, binti huyo mwenye mvuto amesema hakuna mtu wa kumzuia kuwa karibu na Dk. Cheni huku akishikilia alichokisema…. “mambo yetu hayamhusu mtu”, Amani linaandika.
Muda mfupi baada ya Dk. Cheni kusema haoni tatizo kwa kumuoa Lulu, gazeti hili lilimtafuta msanii huyo kwa njia ya simu “Mtu anayesimama na wewe wakati wa shida ndiye rafiki kwa kweli, Dk. Cheni amenisaidia pale ambapo kila mtu alijitenga nami, kama kuna kinachoendelea kati yetu, ni cha kwetu na mambo yetu,” alisema.

0 comments:

Post a Comment