Msanii ambaye yupo chini ya Label ya WCB, Harmonize jana amezawadia gari aina ya Mark X na uongozi wake wa WCB kama motisha kwa kazi zake lakini pia kama njia ya kumrahisishia usafiri na kulinda jina lake na hadhi yake.
Baada ya kupewa zawadi hiyo ya gari msanii huyo alikuwa na maneno ya shukrani kwa uongozi wake huo na kusema kuwa kitendo hicho kimemfanya awe na furaha ambayo hajawahi kuwa nayo.
“Nichukue fursa fupi Kuushukuru uongozi wangu mzima wa WCB Wasafi, Mkubwa Fella, Babutale, Sallam, Ricardomomo pamoja na Diamond Platnumz kwa kunijali na kunithamini kijana wao wakani zawadia gari Daaaaah furaha niliyo nayo haielezeki. Ninafuraha na ninashukuru sana, nina mengi yakuongea lakini sidhani kama nikianza kuandika nitamaliza” alisema Harmonize
Mbali na hilo Harmonize alizidi kutoa shukrani zake kwa wazazi wake kwa kumlea na mashabiki zake ambao wao ndiyo wamempa nguvu zaidi na kusupport kazi zake mpaka sasa
“Nitakuwa mchoyo wa fadhila sisipo washukuru wazazi wangu walio nizaa na kunilea hadi nikafikia hapa na shukrani za dhati ziwafikie mashabiki zangu ambao wapo bega kwa bega kuni support katika kazi zangu pia Mama Naseeb umekuwa ukinisistiza na kunisihi jinsi ya kuishi na watu” alimaliza kwa kusema Harmonize
0 comments:
Post a Comment