Hard way ni filamu kali sana inamhusu kijana Harrison King ambaye ameishi na kulelewa na mzazi mmoja tu ambaye ni Mama, pamoja na yote Harrison ni mtaalamu wa kompyuta. Anafuatwa na kundi la uhalifu linalojulikana kama Triple six wakimtaka atumie uwezo wake wa kompyuta kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti moja kwenda kwenye akaunti nyingine.
Harrison anakataa Triple Six wanamuua mke wake ambaye ni mjamzito, Pamoja na hayo wanamteka Mama mzazi wa Harrisson
Harrison anabaki peke yake anamfuatilia Trace ambaye ndiye mmiliki wa kundi la Triple six ili amwue lakini anagundua kuwa Trace ni dada yake tumbo moja, ni inayokutanisha familia moja katika majanga, Jambazi Trace anagundua kuwa alimuua mama yake mzazi pia anagundua alimuua mke wa kaka yake pamoja na mtoto tumboni ndipo neno la filamu linasoma THE HARD WAY.
Filamu hiyo ambayo ni move bomba sana ambayo inawakutanisha wasanii nyota kama Sydney Van Khanga ‘Harrison’, Aunty Ezekiel aliyeigiza kama Sasha
Possiana Mmasy alicheza kama Tracy wasanii wengine ni Salehe Bagaza, Rashid Fundikira na wasanii waotamba katika soko la Filamu Swahilihood kwa utamu zaidi
Possiana Mmasy alicheza kama Tracy wasanii wengine ni Salehe Bagaza, Rashid Fundikira na wasanii waotamba katika soko la Filamu Swahilihood kwa utamu zaidi
0 comments:
Post a Comment