+10 344 123 64 77

Monday, May 18, 2015

NISHA:: TUACHENI MAMBO HAYA====>>YAPI HAYO FUATILIA

Nisha: Acheni Kuazima vya Watu
     NI Staa wa Bongo Movies, Salma Jabu ‘Nisha’, amewataka mashabiki wake wenye tabia ya kuazima vitu kwa marafiki zao waache kwa kuwa vinaweza kuwaletea madhara makubwa.

    Licha ya somo hilo kulitoa katika filamu yake ya ‘Mtaa kwa Mtaa’, pia ameweka wazi kwamba kuazima nguo ama vitu vingine kunaweza kumkosesha amani ama heshima mwazimaji jambo ambalo litampotezea muda wa kufanya maendeleo.

    “Hilo ni moja ya somo kwenye filamu yangu hiyo, naamini wapo watakaojifunza kulingana na hilo, nimeuvaa uhusika huo ili kutoa somo hilo kwa mashabiki wangu,” alisema.

    0 comments:

    Post a Comment