+10 344 123 64 77

Sunday, June 14, 2015

JOHARI!!!! NI KWELI NINA MTOTO....BABA YAKE NYINYI WA NINI???

Johari: Nina mtoto sawa, mnataka kumjua baba yake ili iweje?
NI YULE Staa wa Bongo Movies, Blandina Chagula  >>Johari<< amedai kushangazwa na watu wanaoshindwa kufanya mambo yao binafsi na kuanza kufuatilia maisha yake pamoja na mtoto wake.

ohari ameiambia Bongo5 kuwa anaishi kwa furaha na mwanae licha baadhi ya watu kumfuatilia na kutaka kujua mtoto wake amezaa na nani kitu ambacho hapendi kukiweka wazi kwa sasa.
“Sidhani kama kuna mtoto ambae anakosa baba,” amesema muigizaji huyo.

“Siku nitapokuwa tayari nitamweka wazi baba yake ili waridhike. Kwa sababu nashangaa watu wanaingilia vitu vyangu private. Katika maisha yangu mimi sio mtu wa matangazo, nianze kutangaza nina mimba! Nimejifungua sina hizo, mimi ninachotaka watu waache kufuatilia privacy yangu, yaani waendelee kufuatia kazi zangu na sio vitu vinavyoandikwa na magazeti ya udaku. Mimi ninachoshukuru Mungu nipo happy pamoja na mwanangu,” ameongeza.

Katika hatua nyingine Johari amesema filamu yake ijayo inaitwa ‘Mapenzi ya kweli hayafi.

“Kuna movie mpya ambayo natarajia kutoa hivi karibuni inaitwa Mapenzi ya kweli hayafi, yaani ‘True love never die’ ambayo nimecheza mimi Irene Uwoya na Single Mtambalike Rich. Hii ni idea ambayo nilipata mimi mwenyewe kichwani kwangu na nikaamua kuifanyia kazi.”

0 comments:

Post a Comment