+10 344 123 64 77

Wednesday, June 24, 2015

MADRID HISPANIA!!!!!! ATLETIKO MADRID YASAJILI WASHABULIAJI WAPYA...............FUATILIA KUJUA NI AKINA NANI HAPA....

Jackson-Martinez

NI>>> Siku chache baada ya kushuhudia mshambuliaji wake raia wa Croatia Mario Mandzukic akihamia nchini Italia kwenye klabu ya Juventus , mabingwa wa Hispania kwa msimu wa mwaka 2013/2014 Atletico Madrid hii leo wamethibitisha kumsajili mshambuliaji raia wa Colombia Jackson Martinez toka Fc P0rto ya nchini Ureno .
Martinez amekuwa akitajwa kwenye vichwa vya habari za michezo akihusishwa na kujiunga na klabu kadhaa kubwa barani ulaya ikiwemo Arsenal na Ac Milan na kuna wakati iliaminika kuwa yuko karibu kujiunga na Ac Milan ambayo imekuwa ikisaka wachezaji wa kurudisha hadhi yake iliyopotea .
Mshambuliaji huyu mwenye umri wa miaka 28 amekuwa na rekodi nzuri ya ufungaji kwenye ligi ya Ureno tangu alipojiunga na Fc P0rto ambapo kwa misimu minne amefunga mabao 67 kwenye ligi huku msimu uliopita akifunga mabao 7 kwenye mechi 8 za michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya ambapo Port0 ilifika hatua ya robo fainali .

0 comments:

Post a Comment