+10 344 123 64 77

Monday, June 1, 2015

MAPENZI!!!!! KWA WALE WENYE WAPENZI AMBAO HAWAJA TULIA......SOMA JINSI YA KUMTULIZA MPENZI WAKO HAPA

HAYA NI MASWALA YA KUZINGATIA SANA ILI KULINDA MAPENZI YAKO.....
KABLA YA YOTE   napenda kukusalimu na kukutakia afya njema maana naelewa mwanamke anapoumwa mambo mengi hudorora yakiwemo malezi ya familia.Baada ya kusema hayo, ngoja nirejee kwenye jambo muhimu nililokuandalia linalohusu mwanamke kujiongeza kwa mumewe na siyo kupita huku na huko kuchonga umbeya.

Kujiongeza ninakokuzungumzia ni kuwa mbunifu wakati wa kula chakula cha usiku maana pamoja na kumfulia nguo, kumpikia, kumfanyia mambo kemkemu lakini bila ya kujiongeza kunako sita kwa sita ni kazi bure.Shoga yangu, kila kukicha kuna wenzetu wanalia kuporwa waume zao na michepuko au akina baba kuwa na nyumba ndogo lakini kiini chake ni baadhi yetu kutojiongeza.
Kama ambavyo nimekuwa nikizungumza mara kwa mara kwamba malovee ni sanaa inayohitaji ubunifu kila kukicha, kama wewe bado unaendesha mapenzi kwa mfumo wa mwaka arobaini na saba, hesabu umeumia.Shoga yangu, malovee kama nilivyowaambia wiki iliyopita ni vionjo, mama mlilie, mdekee, mchombeze mumeo kwa maneno matamu hakika utafurahi na roho yako.



Usidanganyike shoga yangu kwamba mapenzi ni limbwata, hakuna uchawi katika mapenzi ni wewe kujiongeza kwani wataalam wa masuala ya mapenzi wanasema mapenzi ni uchafu ukiona kinyaa huwezi kuyafurahia. 

0 comments:

Post a Comment