Mama huyo alimuunguza mwanaye Joseph Chawala, akimtuhumu Kuiba Ugali, kwa mujibu wa watendaji mbalimbali wa kata ya Mng'eta.
Wakizungumzia tukio hilo Jerome Chulu na Jeneth Hetela, walisema unyanyasaji huo ulishuhudiwa na majirani wa mwanamke huyo baada ya kusikia kelele za watoto ambao walimchukua mtoto huyo kumpeleka of isi ya mtendaji wa kata,polisi na baadaye hospitali.
Walibainisha baadaye kuwa polisi walikwenda kumkamata mwanamke huyo na mumewe Halidi Kiwenji ambaye inadaiwa alikuwa karibu wakati wa tukio hilo ingawa baadaye baba huyo aliachiwa ili akawaangalie watoto wengine nyumbani.
Polisi walithibitisha tukio hilo ambalo uchuguzi wake unaendelea ili kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo.Wananchi mbalimbali waliohojiwa wametaka hatua kuchukuliwà kwa watu wanaoendekeza vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.
0 comments:
Post a Comment