NI HALI si shwari! Mjengo wa staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ uliopo Kimara Saranga, Dar ambao alisema amemzawadia mama yake mzazi, Lucresia Karugila, umezua utata baada ya madai kwamba eti umeshauzwa.
Kwa mujibu wa chanzo ambacho ni jirani mmoja wa eneo hilo, mjengo huo umeuzwa kutokana na uamuzi wa Lulu mwenyewe bila kujulikana sababu licha ya manenomaneno kwamba, mama Lulu alikuwa hataki kuhamia hapo akitaka mjengo mkubwa zaidi kama wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ uliopo Madale, Dar.
Jirani huyo alisema kuwa, ni muda mrefu hajamwona Lulu wala mama yake licha ya kwamba kuna mlinzi wa kulinda nyumba hiyo lakini anaishi nyumba nyingine ya jirani.
0 comments:
Post a Comment