Msanii wa muziki Ommy Dimpoz, ameeleza kuwa wakati wasanii wengine wakiwa na mipango mbalimbali kuukabili mwaka 2016, kwa upande wake akiwa na timu nzito ya wasimamizi, amejipanga kuwa sasa ndiyo wakati wake kutoka na kolabo kubwa za kimataifa.
Dimpoz amesema kuwa, kazi hiyo ambayo pia ni matunda ya usimamizi wake mpya itaanza kuonekana kupitia project yake inayofuata, akiwaandaa mashabiki wake na mtoko wa ‘colaboez’ hizo kubwa kubwa ambazo hata hivyo hakuweka wazi kuwa zitahusisha wasanii gani haswa.
Star huyo amesema, hili litathibitika kupitia rekodi ambayo ataiachia baada ya rekodi yake ya sasa “Achia Body” kupita ambapo kwa kushirikiana na timu ambayo sasa imeongezeka kwa upande wa uongozi wake, nyota huyo anatarajiwa kupiga hatua za uhakika katika mkakati wake huo.
0 comments:
Post a Comment