+10 344 123 64 77

Thursday, January 14, 2016

Korede Bello kamaliza tatizo lake na mwalimu wa chuo nakufanya mtihani …

Baada ya headlines za mwenendo mbaya wa mahudhurio ya chuo kwa staa aliyetoka katika record label ya Mavin Korede Bello, kiasi cha kuingia katika mvutano na mwalimu wake wa chuo, kutokana na kutohudhuria vipindi vya chuo kwa asilimia 70 ndani ya semester.
Korede Bello alikuwa na uwezekano mkubwa wa kukosa kufanya mtihani, ila stori mpya ni kuwa Korede Bello alilazimika kuomba msamaha kwa uongozi wa chuo na kuruhusiwa kuingia katika chumba cha mtihani, licha ya kuwa sheria ya utoro wa kutohudhuria darasani ilikuwa inambana. Korede Bello ambaye kwa sasa anasoma chuo cha  Information Management anayo Diploma ya Mass Communication aliyoipata katika chuo cha Nigerian Institute of Journalism.
df
Wiki moja iliyopita Korede Bello aliingia kwenye headlines baada ya ishu yake ya utoro kuvuja na huenda angekosa kufanya mitihani ya semester hii, January 14 wanafunzi wenzake wamefichua siri kuwa staa huyo aliyeshiriki katika hit single ya Dorobucci na single yake yaGodwin amemaliza matatizo yake na chuo. Kwa sasa Korede Bello yuko kwenye headlines ya hit single nyingine ya Mavins record inayoitwa Jantamanta.

0 comments:

Post a Comment