+10 344 123 64 77

Saturday, January 23, 2016

SHISHI..AMTESA NUHU KWA TATUUUU...

Shilole-na-Nuh-Mziwanda-600x400
Kama huna taarifa basi kaa ukijua kuwa, lile penzi lililokuwa na sarakasi nyingi, mara wafumaniane, mara wapigane, mara waachane sasa limefikia mwisho kama siyo kikomo. Nawazungumzia mastaa wawili, Nuh Mziwanda na Shilole ambao wametangaza rasmi kwamba kila mmoja kuwa na hamsini zake.
Shilole amesema kuwa, haoni sababu ya kuendelea na Nuh kwa kuwa anahisi anambana tu na wala haoni faida kubwa ya kuwa naye.
Kufuatia maneno hayo, Nuh ameona isiwe kesi, amekubali yaishe lakini taarifa iliyotua kwenye ukurasa huu ni kwamba, jamaa anahaha kufuta tatuu aliyojichora mwilini mwake yenye jina la Shilole.
“Kimsingi ile tatuu ya Shilole inamtesa sana Nuh,” alisema rafiki wa msanii huyo.
Nuh anasemaje? Msikie: “Ni kweli ila hii tatuu nitaifuta nitakapompata wa kuziba pengo la Shilole.

0 comments:

Post a Comment