Diamond Platnumz amechukizwa na jinsi wasanii anaowaheshimu wanavyohaingaika kumchafua yeye na mwanae Tiffah mtandaoni na amesema tayari anawajua wasanii hao.
Akizungumza kwa hasia na Ayo TV Alhamisi hii, Diamond alisema anawashangaa wasanii wanaotumia muda mwingi kumponda mtoto wake kuliko kutafuta pesa.
“Watu wamekaa kwenye sanaa muda mrefu mimi nimewakuta, nawaona wameanza kuwa mastaa kabla ya mimi, hawana viwanja, hawana nyumba, hawana magari. Wangetumia muda huo kutengeneza maisha yao kuliko kukaa kumdis mtu mwingine. Halafu mimi sipendagi kusema lakini inavyofika hatua kwenye vitu kama hivi mimi naongea. Kwanza nilikuwa sijui uchungu wa mtoto sasa hivi naujua kwamba kweli mtoto anauma,” alisema Diamond.
“Halafu mtu anayezungumzia inawezekana mtoto akawa na pesa kuliko hata yeye, kwa sababu akaunti ya Tiffah inawezekana ikawa na hela hata kuliko huyo mtu anayemdiss huyo mtoto kama sio wangu mimi. Inawezekana akawa na hela kuliko hata wewe unayesema mtoto sio wangu au unasema mtoto mbaya. Kwa sababu mtoto alifunguliwa akaunti yake kwa mara ya kwanza ikaingia milioni 10. Ni mtoto inawezekana ni maarufu kuliko hata wewe kwa sababu nikifika Nigeria wanaanza kuuliza Tiffah hajambo? So inafikia time hata kwa mtoto unataka kiki?”
“Kwa ndugu zangu wasanii waache kidogo kumfuata fuata binti yangu, kila mtu anakuja sijui DNA sijui nini, waache hizi mambo mimi ndiye mwenye mtoto.”
Tazama mahojiano hayo hapo chini.
0 comments:
Post a Comment