+10 344 123 64 77

Saturday, January 23, 2016

YA NISHA KIBOKO KABISA..INA HESABU SIKU..USIKOSE HII...

KIBOKO KABISA
ILE Filamu ya Kiboko Kabisa kutoka kwa gwiji la Uchekeshaji Swahilihood Salma Jabu ‘Nishabebee’ ipo tayari na inehesabu siku kadhaa ili iruke mtaani na kufanya fujo za hatari huko kunako soko ni kazi safi si ya kuikosa kwani imejaa mastaa kibao.
Akiongea na FC Production meneja wa Nisha’s Film Productions Othuman Ochu amesema kuwa kila kitu kipo tayari ikiwa printing na mzigo umekamilika kwa ajili ya kuingia sokoni tarehe 29.January. 2016 na itapatikana nchi nzima katika maduka ya filamu za Kibongo.
“Filamu ya Kiboko Kabisa imekamilika na ipo kwa ajili ya kuingia sokoni soon na inakuja kuwashika sokoni wale wote waliingiza kazi zao sokoni ni kazi nzuri nay a kipekee kabisa kutengenezwa Bongo,”anasema Ochu.
Sinema ya Kiboko kabisa imetengenezwa na kampuni ya Nisha’s Film productions huku ikiwa imewashirikisha wasanii nyota wanaotamba sokoni kama vile King Majuto, Ben Blanco, Mzee Jengua, Nishabebee na wasanii wakali katika tasnia ya filamu Bongo si ya kuikosa

0 comments:

Post a Comment