+10 344 123 64 77

Wednesday, May 20, 2015

BATULI:: NATAMANI WATOTO MAPACHA======>>>soma zaidi

Batuli Atamani Watoto Mapacha
NI Staa mrembo wa Bongo Movies, Yobnesh Yossuf ‘Batuli’, amesema anatamani kupata watoto mapacha wa kike katika maisha yake.
Akizungumza juzi alipotembelea ofisi za gazeti la Mtanzania, mrembo huyo mwenye watoto wawili wa kiume, alisema moja ya mipango yake ni kupata mtoto mwingine wa kike, tena ikiwezekana mapacha.
“Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia kupata watoto wa kiume wawili, lakini bado nina mpango wa kuongeza wengine wa kike na nitafurahi nikipata mapacha, lakini nikishindwa kabisa nitatumia njia kama wanazofanya wazungu za kuasili,” alisema.

0 comments:

Post a Comment