Huku ishu hiyo ikipingwa vikali na Aunt, washakunaku wa mambo ya watu waliozungumza na Amani baada ya kumuona Cookie walidai kwamba mtoto ni mweupe wakati Moze ni mweusi ‘tiii’.Zengwe hilo lilianza kusambaa miongoni mwa mashosti waliokwenda kumpa hongera Aunt nyumbani kwake, Kinondoni, Dar, saa chache baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini.
>>>Unajua tangu akiwa mjamzito kuna watu walikuwa na shauku ya kumuona mtoto kujua kama kweli ni wa Moze maana mwanzoni hakuna aliyeamini kama mimba ni ya Moze ‘s0’ hao ndiyo wameanza chokochoko,” kilisema chanzo chetu kwa sharti la kutochorwa gazetini.
0 comments:
Post a Comment