+10 344 123 64 77

Friday, May 15, 2015

LULU:: NATAMANI KUIMBA GOSPEL(INJILI) JAMANI

Lulu Atamani Kuimba Injili


    Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema anatamani sana siku moja  kuimba muziki wa injili kwa vile anacho kipaji cha uimbaji.
    Staa huyo aliyasema hayo wakati akihojiwa  kwenye kipindi cha  televisheni cha The Sporah Show wiki hii.
    “Napenda kuimba...nadhani naweza kuimba, napenda kama siku ikitokea nimekuwa muimbaji  niimbe gospel, napenda sana gospel" hayo aliyasema  Lulu.
    Pia Lulu alisistiza kuwa yeye ni mtu mwenye hofu ya Mungu.
    “I’m  God fearing  yaani namuogopa sana na namuheshimu sana Mungu sio kumuogopa peke yake. Kwahiyo pamoja na yote ninayoyafanya  imani yangu ipo palepale hata mungu anajua.
    Mnanijua kwa nje , huo ndio upande mnaoujua, kuna upande wangu wa ndani na hauwezi kuujua lazimu muwe watu wa ndani sio kila mmoja anaweza kuujua”-Lulu alisisitiza.

    0 comments:

    Post a Comment