+10 344 123 64 77

Wednesday, August 12, 2015

MAHUSIANO YA FREEMASONS NA MUNGU YAPOJE??????? JE YAPO KWELI?? BOFYA KUJUA ZAIDI HAPA

Mpenzi msomaji wiki iliyopita niliishia pale nilipokuwa nikielezea uhusiano uliokuwepo baina ya falsfa ya siri ya makuhani wa Misri ya kale na Freemasons wa leo. Utawala wa Misri ya kale ambao unachukuliwa kama utawala wa kisiasa uliomkana Mungu, ulitoweka maelfu ya miaka iliyopita. Je, utawala huo waweza kuwa na athari zozote hivi leo?SONGA NAYO…Katika Kitabu cha Freemasons wenyewe cha The Hiram Key kilichoandikwa na waandishi wa Kimasoni, Christopher Khight na Robert Lomas, jamaa hao wanaeleza kuwa Misri ya kale inachukuwa nafasi muhimu kuhusiana na chimbuko la Freemasonry. Hakuna namna ya kuitenganisha jamii hiyo na Misri ya kale. Kitabu hicho kinaeleza kwamba, lengo la jamaa hao ni kuona ulimwengu unajiendesha wenyewe, yaani kama bahati nasibu bila kuwepo kwa nguvu nyingine ya kitawala duniani ya kuwazidi wao (jamii ya siri).Kwao wao, halikuwa jambo la kimantiki kumfikiria Mungu kuwa ndiye aliyeumba kila kitu. Wao waliamini kwamba dunia ilianza pale utulivu ulipokuja baada ya mparaganyiko wa vitu na kwamba tangu wakati huo kumekuwa na ugomvi kati ya nguvu za umoja na nguvu za utengano, sehemu zote zilikuwa giza totoro, nguvu ya maumbile iliyokuwa ndani yake ikaamuru maisha yaanze.Jamaa hao walieleza kuwa Misri ya kale ndiyo kila kitu katika kuanzishwa kwa Freemasonry. Jamaa hao walifafanua kwamba, kuna uwiano kati ya imani za kale za Misri na sayansi ya leo. Baadhi ya wanasayansi wa leo wakajikuta wakiachana kabisa na Ukristo na kujiundia jumuiya iliyopingana na dini. Wakajikuta wakiingiwa na itikadi ya kipagani ya kizamani kuliko Uyahudi. Kwamba itikadi hii ilitumbukizwa tu katika dini hii na kwamba mizizi yake halisi inaonekana katika Misri ya kale.Kuna maelezo kwamba, Masoni hao waliweka kumbukumbu yao katika historia ya dunia tangu karne ya 18, wakifanya mapinduzi, wakijenga falsafa na mifumo ya kisiasa na ndiyo warithi wenyewe wa wachawi wa Misri ya kale.Katika Kitabu cha Kutoka ambacho ni cha pili cha Torati katika Agano la Kale kwenye Biblia, imeelezwa jinsi wana wa Israel, chini ya uongozi wa Musa walivyohama Misri ya kale kuepuka udhalimu wa Farao.Kama nilivyoeleza huko nyuma, Farao, kupitia washauri wake na Makasisi wa Kimasoni, aliwashurutisha wana wa Israel kuishi kama watumwa na alikataa kuwaachia huru. Lakini alipokumbana na miujiza aliyoonesha mwenyezi Mungu kupitia kwa Musa na maangamizi aliyowapelekea watu wake, Farao alitulia.Kwa hiyo usiku mmoja, wana Israel wakajikusanya na kuanza safari ya kuhama Misri kwenda nchi ya ahadi. Baadaye Farao akawashambulia wana wa Israel lakini Mungu akawanusuru kwa muujiza mwingine alionesha kupitia kwa Musa.Miongoni mwa mambo muhimu kuhusiana na kuhama kwa wana wa Israel kutoka Misri, ni kuwa waliiasi dini iliyofunuliwa kwao na mwenyezi Mungu, licha ya ukweli kwamba, mwenyezi Mungu aliwanusuru na udhalimu wa Farao kupitia kwa Musa.Wana wa Israel hawakuweza kulielewa hilo badala yake wao walizidi kuielekea ibada ya sanamu. Wakamwambia ewe Musa! Tufanyie miungu na sisi yaani masanamu kama wenzetu walivyo na miungu.Lakini Musa aliwajibu, hakika ninyi ni watu mfanyao ujinga akiwatahadharisha kuwa wataangamia.Kwa nini wana wa Israel walikuwa na msimamo wa ukaidi namna hiyo katika kutafuta masanamu na kuyaabudia? Ni nini chanzo cha mwelekeo huu? Je, kuna mkono wa FreemTukutane wiki ijayo kumalizia historia ya jamaa hawa na kuanza sarakasi za namna ya kujiunga nao.



0 comments:

Post a Comment