Salha Israel akiwa na mumewe.
“Awali wale watu walikuwa wanapendana sana lakini cha ajabu kumekuwa na migogoro midogomidogo kwenye ndoa yao hadi kufikia wakati wenyewe wanajiuliza mchawi ni nani ilihali wao wanaonekana wanapendana sana,” kilisema chanzo hicho ambacho ni mtu wa karibu wa wanandoa hao.Baada ya ishu hiyo kutua kwenye dawati la gazeti hili, mwanahabari wetu alianza kwa kumsaka Tiff ambaye alipoulizwa kuhusu taa nyekundu kuiwakia ndoa yake alifunguka kuw anachokijua yeye ni kwamba amepata mke mwema lakini kuna watu wanataka kumharibia ndoa yake huku akimwachia Mungu kumsimamia. “Hakuna asiyejua kama mimi nimepata mke mwema sana lakini kuna watu hawapendi kuona ndoa yangu inaendelea.
Mimi namuachia Mungu kwani yupo pamoja nasi siku zote,” alisema Tiff huku akishindwa kukubali au kukataa kumtwanga talaka Salha. Salha na Tiff walifunga ndoa ya siri ya kiserikali mwaka 2014, nyumbani kwa wazazi wa mrembo huyo, Sinza-Mori jijini Dar, mwaka 2014.
0 comments:
Post a Comment